Surprise Castle
Shinda Kivuli Kinacho Teketeza Afya Na Mafanikio Yako: Gundua Siri YA Kutibika Na Kufanikiwa Maishani

Shinda Kivuli Kinacho Teketeza Afya Na Mafanikio Yako: Gundua Siri YA Kutibika Na Kufanikiwa Maishani - Paperback

$19.99
$22.95
-13%
Quantity
01

Pay over time for orders over $35.00 with

Offers & Perks

Earn 19 points with this purchase

Added to your rewards balance after checkout.

100 points welcome bonus

Create an account and start with extra points.

Join now
Availability:In StockContributor:Robert R. MndemeTheme:Topical/New AgePublish date:6/14/2013Pages:160
Languages:SwahiliPublisher:Vital World ProjectsISBN-13:9789987942138ISBN-10:998794213XUPC:9789987942138Book Category:Mind, Body, SpiritBook Subcategory:HealingBook Topic:Prayer & SpiritualSize:9.00 x 6.00 x 0.37 inchesWeight:0.245Product ID:SCXK2G5VN7
Unajua siri iliyofichika kwenye hisia hasi za woga, shaka, wasiwasi, hasira, chuki, kinyongo na hisia hasi nyingine zote? Umeshajiuliza au kutafakari kwa kina, mahusiano yaliyopo kati ya hisia hasi (negative emotions) na kile kinachoitwa kukosa bahati, maendeleo au kutofanikiwa maishani? Je hisia hizi zina uhusiano gani na matukio hasi kumuandama mtu hadi kumkwamisha kabisa kimaisha? Unajua ni kiasi gani cha uharibifu wa kinga ya mwili kinachofanywa na hisia hizi? Unajua siri iliyopo kati ya hisia hizi na usugu wa magonjwa au magonjwa mapya? Unajua nini kuhusu chimbuko la afya ya asili toka ndani yako mwenyewe; inavyokwamishwa na kuteketezwa na hisia hasi? Unapoelimika na kuerevuka kwa kina kuhusu dhana nzima ya hisia hasi kwenye mchakato wa maisha yako (emotional intelligence), unazinduka na kutambua kwamba, kuwa na afya yote na kufanikiwa maishani ni jambo lisilopingika kwa namna yeyote, na ni haki yako ya msingi kama mwanadamu inayopatikana hata kama umezungukwa na mazingira magumu kiasi gani. Unapozinduka toka kwenye usingizi wa kiufahamu (hypnotic sleep) unaosababishwa na kupumbazwa na hisia hasi, unatambua kuwa afya ya msingi inayotafutwa kote duniani, haianzii kwenye aina yeyote ya dawa, wala nje kwenye mazingira yako, bali inaanzia ndani kabisa kwenye shina la ufahamu unaojenga utu wako, ulio uasili wa mwanadamu. Unapokomaa kwenye utambuzi mpya baada ya kujikomboa kutoka kwenye kivuli kizito kilichojengwa na hisia hasi, unaelewa kuwa ufahamu unaoasilisha utu wako ni nyezo ya kazi, uzalishaji na ustawishaji wa jamii iliyopevuka na kustaarabika. Unatambua pia kuwa ufahamu huo ni chombo cha kuasisi na kurutubisha maadili ya utu wa mtu, kuanzia kwa mtu mmoja, familia hadi ukombozi wa kupatikana kwa Utu wa Taifa la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Languages:SwahiliPublisher:Vital World ProjectsISBN-13:9789987942138ISBN-10:998794213XUPC:9789987942138Book Category:Mind, Body, SpiritBook Subcategory:HealingBook Topic:Prayer & SpiritualSize:9.00 x 6.00 x 0.37 inchesWeight:0.245Product ID:SCXK2G5VN7
Robert R Mndeme ni mwanasayansi mtafiti kwenye nyanja ya maikrobiolojia, madawa na kemikali mbalimbali na baadaye kujikita kwenye nyanja ya tafiti za hisia za mwanadamu katika kuendeleza na kujenga afya na ustawi wa jamii. Amesoma University of Dar es salaam na Alternative Medicine College of Canada na kufanya kazi katika taasisi ya utafiti wa viuatilifu vya nchi za joto Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) na sasa katika kampuni ya Vital World Projects (VWP) inayojihusisha na maendeleo na afya ya ustawi wa jamii. Ameandika machapisho na vitabu kadhaa. Kupitia njia mbalimbali, hutoa ushauri, mafundisho, semina, makongamano na mikutano mbalimbali juu ya ustawi na afya ya jamii ambayo inasadikiwa kupatikana tu kupitia kufuta ujinga, kuelimika na kuelewa kwa undani hisia za chuki, hasira, woga, shaka, wivu, kinyongo na hisia hasi (negative emotions) nyingine zote na vimelea vyake(emotional parasites); zinavyoweza kumtawala na kumdhuru mwanadamu kwenye kila nyanja ya maisha yake. Wasiliana: rmndeme@yahoo.com, www.twitter.com/RobertMndeme na www.duniahai.co
Publisher: Vital World Projects

Free shipping on orders over $75. Standard shipping takes 3-7 business days. Eligible items may be returned within 30 days of delivery. Conditions apply.